Matumaini ya Manchester United
kunyakua taji la ubingwa wa Ligi ya Kandanda ya England yalitiwa doa
wakati Everton ilipopigana kiume wakiwa nyuma ya mabao 4-2 na kumaliza
mchezo kwa sare ya mabao 4-4 katika mpambano wa kusisimua hasa dakika za
mwisho kwenye uwanja wa Old Trafford.
Rooney alionekana kuipatia ushindi Man United alipopachika bao la nne na muda mfupi baadae Everton wakacharuka na kupachika mabao mawili katika muda wa dakika tatu kupitia kwa Jelavic na Steven Pienaar.
Katika dakika za mwisho, Patrice Evra alipiga mpira wa kichwa uliogonga mlingoti wa lango la Everton akiwa karibu kabisa na baadae mlinda mlango wa Everton Tim Howard aliokoa kwa ustadi mkubwa mkwaju wa Rio Ferdinand na kuinyima ushindi Manchester United.
Manchester United hata hivyo bado wanaongoza Ligi Kuu ya England wakiwa na pointi 83
No comments:
Post a Comment