Iran inasema imeanza kuunda
ndege ya ujasusi sawa na ile ya aina ya Sentinel ya Marekani, ambayo
ilianguka nchini Iran mwaka jana.
Wakuu wa Iran wanasema wamepata maelezo kuhusu namna ndege hiyo inavofanya kazi, kwa kufumbua fumbo la software yake; na sasa inaelewa kikamilifu muundo wa ndege hiyo.
Kuna wasiwasi kuwa Iran huenda ikaweza kuigiza rangi maalumu ambayo inasaidia kufanya ndege hiyo isionekane na vyombo vya radar.
Ndege hiyo ya aina ya Sentinel isiyohitaji rubani, inatumiwa sana na Marekani kugundua maficho ya makundi ya wapiganaji nchini Afghanistan na Pakistan.
No comments:
Post a Comment