Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akisalimiana na Waziri Mkuu wa zamani , Edward Lowassa wakati wa Ibada ya kumkumbuka aliyekuwa Waziri Mkuu, hayati Edward Moringe Sokoine, iliyofanyika Kanisa Katoliki, Kigango cha Wami Sokoine, Morogoro Aprili 12, 2012. Watatu Kushoto ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akiongozana na Askofu wa Jimbo Katoliki la Morogoro, Telsphor Mkude baada ya Ibada ya kumkumbuka ya aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Moringe Sokoine, iliyofanyika kwenye Kanisa Katoliki, Kigango cha Wami Sokoine. Wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera na watatu kulia ni Binti wa Marehemu Soine, Namelok Sokoine, ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM)
Baadhi ya washiriki wa Ibada ya kumkumbuka ya aliyekuwa Waziri Mkuu, hayati Edward Moringe Sokoine, wakishiriki katika Ibada hiyo, kwenye Kigango cha Kanisa Katoliki cha Wami Sokoine, Morogoro Aprili 12, 2012.
Askofu wa Jimbo Katoliki la Morogoro, Mhasham Telsphor Mkude, akibariki sanamu ya aliyekuwa Waziri Mkuu, hayati Edward Moringe Sokoine, kwenye viwanja vya Kigango cha Kanisa hilo, katika kijiji cha Wami Sokoine , Morogoro baada ya kuongoza Ibada ya kumkumbuka ya kiongozi huyo.
Askofu wa Jimbo Katoliki la Morogoro, Telsphor Mkude, akiteta ambo na Namelok Sokoine, Binti wa aliyekuwa Waziri Mkuu, hayati Edward Moringe Sokoine, ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum CCM, wakati wa Ibada ya kumkumbuka kiongozi huyo juzi.

No comments:
Post a Comment