Mkurugenzi wa Kuratibu na Kukuza Utafiti wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu(NIMR) Dk. Julius Massaga, akitoa ufafanuzi leo, jijini Dar es Salaam, kuhusu chanjo ya satarani ya shingo ya kizazi kwa wanawake wakati wa semina kwa waandishi wa habari. (Picha na Tiganya Vincent- MAELEZO- Dar es Salam)
Mtafiti Mkuu wa Utafiti wa Chanjo ya kuzuia saratani ya njia ya kizazi wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), tawi la Mwanza Dk. Deborah Waston Jones, akiongea na waandishi wa habari, Dar es salaam leo, kuhusu matokeo ya utafiti wa mapokeo ya wananchi yahusuyo chanjo ya saratani ya njia ya kizazi kwa wanawake . Kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) tawi la Mwanza Dk. John Changalucha.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), tawi la Mwanza Dk. John Changalucha akiongea na waandishi wa habari, wakati wa semina hiyo, jijini Dar es Salaam kuhusu matokeo ya utafiti huo. Kushoto ni Mtafiti Mkuu wa Utafiti wa Chanjo ya kuzuia saratani ya njia ya kizazi wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), tawi la Mwanza Dk. Deborah Waston Jones.


No comments:
Post a Comment