TANGAZO


Friday, April 13, 2012

Mkazi wa Mwanza ajishindia sh. milioni 10, Vodacom M-Pesa



Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu, akiongea na waandishi wa habari, dar es Salaam leo, wakati wa kuchezeshwa droo kubwa ya mwezi ya kumpata mshindi wa sh. milioni 10, katika promosheni ya Vodacom, M-PESA, ambapo mkazi wa Kitangiri, mkoani Mwanza, Revocatus Mkama amejishindia fedha hizo. Jumla ya shilingi Milioni 300, zimetolewa kwa washindi wa promosheni hiyo, tangu kuanza kwa promosheni hyo. Kulia ni mtaalamu wa Huduma za ziada kwa wateja wa Vodacom, Reenu Verma. (Picha na Mpigapicha wetu)



Mtaalamu wa Mawasiliano ya Teknologia wa Vodacom Tanzania, Tulisindo Rashid (kushoto), akifuatilia jinsi komputa inavyochezesha nambari za washiriki wa droo hiyo kubwa ya mwezi kwa ajili ya kumpata mshindi wa sh. mlioni 10 wa promosheni ya M-PESA, ambapo Revocatus Mkama wa Mwanza amekuwa mshindi wa  fedha hizo. Kushoto  ni Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini, Bakari Maggid, Meneja Mawahusiano Matina Nkurlu na Mtaalamu wa Huduma za Ziada kwa wateja wa Vodacom, Reenu Verma.



Meneja Mahusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu, akionesha nambari ya mshindi wa droo hiyo ya mwezi ya kumpata mshindi wa sh. milioni 10 wa promosheni ya M-PESA. Kushoto ni Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini, Bakari Maggid na kulia ni Mtaalamu wa Huduma za Ziada kwa Wateja wa Vodacom, Reenu Verma.

No comments:

Post a Comment