TANGAZO


Wednesday, April 25, 2012

Naibu Waziri Kitwanga afungua mkutano wa Umoja Taasisi za Mawasiliano SADC


Naibu Waziri wa Sayansi na Mawasiliano, Charles Kitwanga, akifungua mkutano wa 32 wa mwaka wa Umoja wa Taasisi za Mawasiliano, Kusini mwa Afrika (SADC), unaofanyika kwa siku mbili na kujadili mambo mbalimbali kuhusu mawasiliano ya simu, ikiwa ni pamoja na mabadiliko ya mfumo wa kidigitali. Mkutano huo unahudhuriwa na wajumbe kutoka nchi 14 za SADC, zikiwemo Zimbabwe, Namibia, Botswana, Malawi Msumbiji, Afrika Kusini, Lesotho na Tanzania. (Picha na mpigapicha wetu)



 Naibu Waziri wa Sayansi na Mawasiliano Charles Kitwanga, akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuufungua rasmi mkutano huo leo jijini.


 Naibu Waziri wa Sayansi na Mawasiliano, Charles Kitwanga, akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa mkutano huo.


 Mkurugenzi Mtendaji wa TTCL, Said Amir Said, akimkaribisha Naibu Waziri wa Sayansi na Mawasiliano Charles Kitwanga ili kufungua mkutano huo.


Wajumbe kutoka nchi mbalimbali za Kusini mwa Afrika (SADC), wakiwa katika mkutano huo, wakimsikiliza Naibu Waziri Kitwanga, wakati alipokuwa akiufungua mkutano wao.


Baadhi ya wajumbe mbalimbali kutoka nchi za SADC, wakiwa katika mkutano huo, wakifuatilia hotuba ya Naibu Waziri Kitwanga.


 Wajumbe kutoka nchi mbalimbali za SAADC, wakiwa katika mkutano huo, wakati Naibu Waziri Kitwanga, akiufungua mkutano wao.


 Baadhi ya wajumbe wa nchi mbalimbali kutoka nchi za SAADC, wakiwa katika mkutano huo.

No comments:

Post a Comment