Mwanamitindo Gura (kushoto), akiwa na Millen Magessa |
Na Mwandishi Wetu
MWANAMITINDO Anastazia Gura aliyechaguliwa na mbunifu mkubwa wa mavazi wa Afrika Kusini
Olive Clandle kuonesha mavazi yake ameeleza kufurahishwa na hatua hiyo.
Anastazia
akihojiwa na waandishi wa habari wa hapa Afrika Kusini alisema kuwa akiwa kama
mwanamitindo chipukizi kuchaguliwa kuonesha mavazi ya mbunifu huyo ni hatua
kubwa kwake.
Alisema kuwa kwa
kitendo cha kuchaguliwa bila hata ya kuonekana katika jukwaa ni dhahiri kuwa
anavya vigezo vya kutosha na hivyo amepania kufika mbali zaidi.
Anastazia
alichaguliwa mara tu baada ya kuonekana akijaribisha nguo za wabunifu wa
kitanzania wanaoshiriki katika onesho hilo la wiki ya mavazi.
Alifika nchini
Afrika Kusini kwa lengo la kuonesha mavazi ya wabunifu watatu wa kitanzania
waliochaguliwa na mwanamitindo wa kimataifa Millen Magese.
Lakini hata hivyo
alijikuta akichaguliwa kuonesha na mavazi ya mbunifu Olive Clande huku akiwa
ndio kwanza anaingia katika tasnia ya uanamitindo huku akiwa hajawahi hata kutembea jukwaani.
Hatua hiyo
imeonekana kuwashangaza waandishi wa habari wa mitindo na hata wanamitindo
wengine waliopo hapa Afrika Kusini kwa kuwa mara zote mbunifu huyu hupendelea
kuwatumia wanamitindo wenye majina makubwa.
Akizungumzia hatua
hiyo Millen alisema kuwa Anastazia na vigezo vyote vinavyotakiwa kuwa
mwanamitindo na ndio maana ameweza kupatiwa nafasi hiyo kirahisi.
“Ni kwamba ili
uweze kuchaguliwa inatakiwa angalau uwe na vigezo vya kimataifa ili kumwezesha
mbunifu kuchagua mtu wa kumuoneshea nguo zake” alisema Millen.
No comments:
Post a Comment