Mtu maarufu wa kabila la Wasukuma, ajulikanaye kwa jina la "Mchoma Simba", ambaye huvishwa mavazi hayo baada ya kuua Simba, kama ishara ya ushujaa, akicheza ngoma mbele ya uongozi wa Mkoa ya Rukwa na Mkoa mpya wa Katavi, wakati wa makabidhiano ya Mkoa huo jana. Mkoa wa Rukwa umegawanywa na kuanzishwa Mkoa wa Katavi, ikiwa ni jitihada za Serikali katika kusogeza huduma kwa wananchi wake. Kutoka kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima, Mkuu wa Mkoa Mpya wa Katavi Dk. Rajab Mtumwa Rutengwe, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Injinia Stella Manyanya na Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Joyce Mgana. (Picha na mpiga picha wetu)
Mkuu wa Mkoa mpya wa Katavi Dk. Rajab Mtumwa Rutengwe, akiwa ameketi kwenye kigoda, akiombewa dua na Chifu wa kabila la Wabende, Chifu Victor Mfinula, kabla ya kutunukiwa Uchifu wa kabila hilo jana, baada ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa kwanza wa Mkoa mpya wa Katavi.
Katibu Tawala wa Mkoa mpya wa Katavi, Injinia Emmanuel Kalobelo, Mkuu wa Mkoa huo, Dk. Rajab Mtumwa Rutengwe, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Injinia Stella Manyanya na viongozi wengine wakiwa kwenye moja ya Sala zilizoongozwa na viongozi wa Dini waliohudhuria hafla hiyo.
Wananchi wa Katavi, walijitokeza kwa wingi kuwalaki kiongozi wao, Mkuu wa Mkoa huo, Dk. Rajab Mtumwa Rutengwe na Katibu Tawala wa Mkoa huo, Injinia Emmanuel Kalobelo.
Eneo la mpaka la Mikoa ya Rukwa na Katavi, kwenye mlima maarufu wa Lyamba Lyamfipa ambapo Utawala wa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Injinia Stella Manyanya unaishia, anashusha bendera, kuruhusu Utawala Mpaya wa Dk. Rajab Mtumwa Rutengwe, kupandisha bendera yake, tayari kuipeperusha kwenye Milima na Mabonde ya Utawala wake mpya wa Mkoa mpya wa Katavi.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Injinia Stella Manyanya, akihutubia wananchi wa Mkoa mpya wa Katavi, waliojitokeza kwa wingi, kabla ya kuwatambulisha viongozi wao katika uwanja wa mpira wa Kashaulili uliopo wilayani Mpanda. Injinia Manyanya, aliwaomba wananchi hao, kuwapa viongozi wao hao, ushirikiano wa dhati ili kurahisisha utendaji kazi wao kwa maendeleoa ya Katavi na ukanda mzima wa Ziwa Tanganyika.
Mkuu wa Mkoa mpya wa Katavi Dk. Rajab Mtumwa Rutengwe, akihutubia wananchi wake wa Mkoa mpya wa Katavi mara baada ya kutambulishwa kwao na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Injinia Stella Manyanya. Aliwaahidi ushirikiano wa hali na mali kuhakikisha Katavi inasonga mbele.
Safari ya kuelekea makabidhiano ilianza ofisini kwa Mkuu wa Mkoa Rukwa, Injinia Stella Manyanya ambaye alianza kwa kumuombea dua Mkuu wa Mkoa mpya wa Katavi Dk. Rajab Rutegwe mapema kabla ya kuanza safari kuelekea wilayani Mpanda, Mkoa mpya wa Katavi, ambapo ndipo yalipofanyika makabidhiano hayo. Mkoa wa Rukwa umegawanywa na kuundwa Mkoa mpya wa Katavi, ikiwa ni juhudi za Serikali katika kusogeza huduma zake kwa wananchi. Kwa pamoja viongozi wote wa Mikoa ya Rukwa na Katavi wameishukuru sana Serikali ya Dk. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuugawa Mkoa wa Rukwa kwa maslahi ya wananchi wake.
No comments:
Post a Comment