TANGAZO


Tuesday, April 3, 2012

Mkutano wa Wadau wa Bima ya Afya Kilimanjaro


Naibu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Hamis Mdee akitoa maelezo ya Utangulizi juu ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na Mfuko wa Afya ya Jamii wakati wa Mkutano wa wadau wa NHIF na CHF mjini Moshi. (Picha na Mpigapicha wetu)

Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya NHIF  ambaye pia ni Mhasibu Mkuu wa Serikali Mama Mwanaidi Mtanda akiongea wakati wa Mkutano wa Wadau wa NHIF na CHF Mjini Moshi.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Lawrence Gama, akifungua rasmi mkutano wa Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) wa Mkoa wa Kilimanjaro uliofanyika jana katika ukumbi wa Uhuru Hotel. 


Wadau mbalimbali wa NHIF na CHF, wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa katika Mkutano wa wadau wa Mifuko hiyo, mjini Moshi. Mkutano huo ulijumuisha wadau wapatao 280, kutoka wilaya zote za Mkoa huo.


Mkuu wa Wilaya ya Same, Marwa, kama mdau mmojawapo wa NHIF, akichangia mawazo juu ya kuboresha huduma za CHF katika Halmashauri za Mkoa wa Kilimanjaro katika mkutano wa wadau wa NHIF uliofanyika mjini Moshi.

No comments:

Post a Comment