Mmoja wa wanakijiji cha Mtunduwalo, John Nyimbo, akitoa maelezo juu ya malalamiko yao kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu (hayupo pichani), kuhusu kulipwa fidia kidogo ya ardhi waliyoitoa kupisha mradi wa mgodi wa makaa ya mawe wa Ngaka, wilayani humo.
Wananchi wa kijiji hicho, wakisikiliza kwa maelekezo ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Said Mwambungu (hayupo pichani), kuhusu malalamiko yao ya kulipwa fidia ndogo ya maeneo yao, kupisha mradi wa makaa ya mawe wa Ngaka hivi leo.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Said Mwambungu, akiagana na wanakijiji hicho, baada ya kumalizika kwa mkutano wake na wanakijiji hao.

No comments:
Post a Comment