TANGAZO


Tuesday, April 3, 2012

Waasi wa Tuareg wasonga kati ya Mali


Mpiganaji wa Tuareg
Waasi wanaoongozwa na Watuareg-wamesonga mbele hatua mbele katika maeneo ya Kaskazini ya Mali, eneo kubwa wanalodai liwe huru. Hali ya wasiwasi inazidi kuongezeka kuhusu harakati za makundi ya wapiganaji wa Kiislamu Kaskazini ya Mali baada ya waasi wanaoongozwa na Watuareg kuyateka maeneo makuu ya eneo hilo mnamo wiki iliyopita. .
Waasi hao wakiongozwa na makamanda watuareg wameteka maeneo zaidi katika mkoa wa kati wa Mopti kwa mujibu wa wakaazi wa eneo hilo waliowasiliana kwa njia ya simu. Wameingia katika mji mdogo wa Hombori ulio kilometa 300 Kaskazini mwa mji mkuu wa mkoa wa Mopte bila ya mapigano yoyote .
Awali walisema mji wa Homboni hauko katika eneo la Azawad wanalodai liwe huru. Hakuna ishara yoyote kama watasonga mbele kuelekea kusini. Wapiganaji wa kundi la Waislamu la Ansar Eddine wameanza kutekeleza kanuni za sheria za kiislamu katika miji mikuu mitatu iliyotekwa na waasi mwishoni mwa wiki iliyopita.
Taarifa kutoka Kidal Gao na Timbuktu zaeleza kua wapiganji wa Ansar Edinne walishambulia baa zinazouza pombe na kupiga marufuku kucheza muziki wa nchi za Magharibi katika vituo vya redio. Shirika la Utamaduni la umoja wa mataifa limeelezea wasiwasi wao kua maeneo ya kale katika Timbuktu huenda yakaharibiwa na uasi huo.
Waasi Wanaongozwa na kundi kuu la Watuareg la MNLA,wamekanusha kua na fungamano zozote na Ansar Edine licha ya kwamba makundi yote mawili yameshawahi kushirikiana mara kadhaa katika mapigano.
Makundi haya yanatofautiana katika malengo yao. Kundi la MNLA likidai kupigania uhuru wa kaskazini bila ya fungamano zozote za kidini huku Ansar Edine likitaka kuweka mfumo wa sheria za kiislamu nchini kote na hii kuzusha khofu ya kuzuka.

No comments:

Post a Comment