TANGAZO


Tuesday, April 3, 2012

Mfuko wa Pensheni wa LAPF waisaidia kambi ya masumbwi

 Meneja Mawasiliano na Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, Andrew Kuyeyana (kulia), akikabidhi baadhi ya vifaa vya mchezo wa Masumbwi kwa Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo Taifa (BMT), Henry Lihaya kwa ajili ya mabondia wanaojiandaa kufuzu mashindano ya Olimpic, Dar es Salaam leo.  Kushoto ni  Katibu wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Nchini (BFT), Makore Mashaga. (Picha na Super D, Mnyamwezi)




Katibu wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Nchini (BFT), Makore Mashaga (kushoto) na Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo Taifa (BMT), Henry Lihaya (katikati), wakivifurahia vifaa hivyo. Kulia ni Meneja Mawasiliano na Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, Andrew Kuyeyana.




Meneja Mawasiliano na Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, Andrew Kuyeyana (kulia) akimkabidhi baadhi ya vifaa vya mchezo huo, Katibu wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Nchini (BFT), Makore Mashaga kwa ajili ya mabondia hao. Katikati ni Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo Taifa (BMT), Henry Lihaya. 


Meneja Mawasiliano na Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, Andrew Kuyeyana (kulia), akiwakabidhi moja ya fulana za mazoezi, Katibu wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa nchini (BFT), Makore Mashaga (kushoto) na Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo Taifa (BMT), Henry Lihaya, wakati wa hafla hiyo.

No comments:

Post a Comment