TANGAZO


Tuesday, April 3, 2012

Machinga waondolewa Ubungo Mataa

 Polisi na Askari wa jiji, wakiwa kwenye eneo walilokuwa wakifanyia biashara, wafanyabiashara ndogo ndogo wa Ubungo Mataa, baada ya kuwaondoa katika eneo hilo, linalomilikiwa na Shirika la Umeme nchini (Tanesco), Dar es Salaam leo asubuhi. (Picha zote na Kassim Mbarouk)


 Maofisa wa Jeshi la Polisi, wakijadiliana jambo, wakati wa zoezi la kuwaondoa wafanyabiashara hao, kwenye eneo hilo.


 Vijana wafanyabiashara ndogo ndogo, wakiwa wamejikusanya kando kando ya barabara ya Mandela, karibu na daraja la Ubungo, baada ya kutimuliwa katika eneo walililokuwa wakifanyia shughuli zao, maeneo ya Ubungo Tanesco, Dar es Salaam.




 Askari wa kutuliza ghasia (FFU), wakiwa wamebarizi na gari leo, wakiweka doria ya nguvu karibu na daraja la Ubungo kwa ajili ya kuwakabili wafanyabiashara hao ikitokea kutaka kuleta fujo.



 Wananchi wakiangalia kioo cha gari kilichopigwa jiwe na baadhi ya wafanyabiashara ndogo ndogo wa Ubungo Mataa, karibu na daraja la Ubungo.





Baba wa mmiliki wa gari lililopigwa jiwe na wafanyabiashara hao, akimuonesha Askari wa Usalama Barabarani, eneo walipokutana na kadhia hiyo. 

No comments:

Post a Comment