Kijana mwendesha pikipiki, akijitahidi kujinasua baada ya kupata ajali ya kugongwa na gari ndogo, maeneo ya Kagera, makutano ya barabara za Morogoro na Mburahati, Dar es Salaam leo mchana. (Picha zote na Kassim Mbarouk)
Mwendesha pikipiki, akiangalia madhara aliyoyapata kwenye mguu wake katika ajali hiyo.
Mwendesha pikipiki, akilalamika jinsi ilivyotokea ajali hiyo, huku akiwa amezungukwa na wananchi waliokwenda kumwangalia kwa ajili ya kutaka kumpatia msaada.
Wananchi wakiiangalia pikipiki yake iliyogongwa na gari katika ajali hiyo.
Mwendesha pikipiki, akilalamika kutokana na maumivu anayoyapata kwenye mguu wake wa kushoto.
Mwendesha pikipiki, akibebwa ili kuingizwa kwenye gari lililomgonga kwa ajili ya kukimbizwa hospitali.
Askari wa Usalama Barabarani, akifungua mlango wa gari lililomgonga mwendesha pikipiki huyo.
No comments:
Post a Comment