TANGAZO


Sunday, April 22, 2012

Mkutano wa Chadema mjini Sengerema watia fora

 Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbroad Slaa, akihutubia umati wa wananchi pamoja na wanachama wa Chama hicho katika mkutano uliofanyika mjini Sengerema leo. (Picha na mpigapicha wetu)

Mwanachama mpya wa Chadema, Kamis Mwagao 'Tabasamu', akikabidhiwa kadi yake na Katibu Mkuu, Dk. Wilbroad Slaa katika mkutano huo baada ya kujiunga nacho jana, mjini Sengerema.


 Kijana ambaye hakufahamika jina lake, akiwa amenyanyua bago lenye ujumbe, usemao 'Dk. Slaa tuone tulivyochakaa kwa sababu ya kukosa ajira', katika mkutano uliofanyika mjini Sengerema leo.


 Aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, akihutubia wanachi wa Sengerema jana.


 Aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, akifuta viatu vyake kwa kutumia vitambaa vya bendera na skafu za Chama Cha Mapinduzi (CCM), zilizorejeshwa na waliokuwa wanachama wa chama hicho. 

 Wananchi wakienda kurudisha kadi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. wilbroad Slaa.


 Umati wa wananchi pamoja na wanachama wa Chadema, ukisikiliza hotuba mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwenye mkutano huo.


 Baadhi ya wananchi waliofurika kwenye mkutano huo, wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakitendeka kwenye mkutano huo.


 Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Slaa, akiwa amemkumbatia kijana aliyekuwa amehudhuria kwenye mkutano wake huo, mjini Sengerema.


Hamis Mwagao 'Tabasamu', akizungumza baada ya kukabidhiwa kadi yake ya Chadema kwenye  mkutano huo jana.

No comments:

Post a Comment