TANGAZO


Sunday, April 22, 2012

Rais Kikwete, Shein, Karume wamuaga Mwakanjuki, Shein aongoza mazishi yake

 Rais Jakaya Kikwete, akitoa heshima za mwisho kwa Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu Adam Mwakanjuki, mapema leo asubuhi, April 22, 2012 katika kambi ya JWTZ, Kikosi cha Anga kabla ya kupelekwa Zanzibar kwa mazishi. (Picha na Ikulu)


 Rais Jakaya Kikwete akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu Adam Mwakanjuki mapema leo, asubuhi jijini Dar es Salaam kabla ya kusafirishwa kupelekwa Zanzibar kwa mazishi.


 Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange na Mwakilishi wa Baraza la Wawakilishi, Mohammed Aboud, wakiangalia wakati jeneza lenye mwili wa marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu Adam Mwakanjuki, likipelekwa kwa ajili ya kuingizwa kwenye ndege leo asubuhi, katika kambi ya JWTZ, Kikosi cha Anga kabla ya kupelekwa mjini Zanzibar kwa mazishi.


 Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange na Mjumbe wa Baraza la Wawakilshi wakiangalia jenenza lenye mwili wa Bregedia Jenerali mstaafu, Adam Mwakanjuki, lilipokuwa likiingizwa kwenye ndege, tayari kusafirishwa kupelekwa Zanzibar kwa  mazishi.


 Wanajeshi wa JWTZ, wakiwa wamlibeba jenenza lenye mwili wa marehemu Brigedia Jeneral Adam Mwakanjuki baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Karume, mjini Zanzibar, ukitokea Dar es Salaam kwa ajili ya mazishi leo.


 Wanafamilia wa Marehemu Brigedia Jenerali  Adam Mwakanjuki wakiwa na huzuni baada ya kuwasili kwa mwili wa marehemu huyo, huko Uwanja wa Ndege wa Abeid Karume mjini Zanzibar leo.

 

 Wanajeshi wa JWTZ, wakiwa wamebeba jenenza lenye mwili wa marehemu Adam Mwakanjuki mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Abeid Karume Zanzibar ukitokea Dar es Salaam kwa ajili ya mazishi.


Mwili wa marehem Brigedia Jenerali  Mwakanjuki ukiwa kwa Dada yake Teresa Mwakanjuki huko,Kikwajuni mjini Zanzibar ambapo dada huyo aliuaga.


 Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwawameubeba Mwili wa Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu AdamMwakanjuki,na kuingia katika viwanja vya ukumbi wa zamani wa Baraza laWawakilishi Mnazi mmoja Mjini Unguja leo,ambapo Viongozi mbali mbali na wananchi pamoja na ndugu na jamaa walitoa salamu zao za mwisho kwa mwili wa marehemu Mwakanjuki.


 Baadhi ya wananchi,Jamaa na ndugu wa Marehemu waliofika kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Brigedia Jeneral mstaafu Adam Mwakanjuki katika viwanja vya zamani vya Baraza la Wawakilishi, mjini Zanzibar leo.


 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akitia saini kitabu cha maombolezo ya marehemu Brigedia Jenerali mstaafu Adam Mwakanjuki kwenye ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi Mmoja mjini Unguja. Marehemu amezikwa katika makaburi ya Mwanakwerekwe.


 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohammed Shein akiuaga mwili wa Marehemu Brigedia Jenerali Adam Mwakanjuki katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani Kikwajuni. (Picha na Yussuf Simai-Maelezo Zanzibar 22-04-2012)


Mke wa marehemu Brigedia Jenerali Mwakanjuki Ikupa Abel Mwasongwe akiwa pamoja na Familia yake huko katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani ambako mwili huo umeagwa.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimpa pole mjane wa Marehemu Brigedia Jejerali mstaafu Ikupi Adam Mwakanjuki,wakati wa kutoa  heshima za mwisho kwa mwilli wa marehemu, Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi Mmoja mjini Unguja. (Picha na Ramadhan Othaman, Ikulu)


 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiwapa pole watoto  wa Marehemu Brigedia Jejerali mstaafu Adam Mwakanjuki,wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu,Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilshi Mnazi mmoja Mjini Unguja leo. (Picha na Ramadhan Othaman, Ikulu)


 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiwapa pole jamaa na ndugu wa Marehemu BrigediaJejerali mstaafu,Adam Mwakanjuki,wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu,Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilshi,Mnazi Mmoja mjini Unguja leo. (Picha na Ramadhan Othman, Ikulu)


 Wanafamilia wa Marehemu Brigedia Jenerali  Adam Mwakanjuki wakiwa na huzuni baada ya kuwasili kwa mwili wa marehemu huyo huko katika Uwanja wa Ndege wa Abeid Karume mjini Zaibar leo.

 Spika wa Baraza la Wawakilishi Pandu Ameir Kificho akisaini kitabu cha maombolezo huko katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani ambako mwili huo ulipoagwa.

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd akisaini kitabu cha maombolezo cha Marehem Brigedia Jenerali Mwakanjuki huko katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani ambako mwili huo ulipoagwa. (Yussuf Simai-Maelezo Zanzibar 22-04-2012)


 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd akiuaga mwili wa Marehemu Brigedia Jenerali Adam Mwakanjuki katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani Kikwajuni.


 Rais Mstaafu wa Zanzibar Aman Abeid Karume akisaini kitabu cha maombolezo cha Marehem Brigedia Jenerali Mwakanjuki huko katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani ambako mwili huo ulipoagwa.


 Mke wa Rais Mstaafu wa Zanzibar Shadya Karume akisaini kitabu cha maombolezo cha Marehem Brigedia Jenerali Mwakanjuki huko katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi wa zamani Kikwajuni ambako mwili huo ulipoagwa.

 Rais Mstaafu wa Zanzibar Aman Abeid Karume na Mke wake Shadya wakiuaga mwili wa Marehemu Brigedia Jenerali Mwakanjuki huko katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani ambako mwili huo ulipoagwa. (Yussuf Simai-Maelezo Zanzibar 22-04-2012)



 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akiwa na shada la maua kwa ajili ya kuliweka kwenye kaburi la marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu Adam Clement Mwakanjuki,wakati wa mazishi yake kwenye makaburi ya Mwanakwerekwe Mjini Zanzibar.(Picha na Ramadhan Othman IKULU)


 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiweka shada la mauwa katika kaburi la marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu Adam Clement  Mwakanjuki,wakati wa mazishi yake yaliyofanyika leo katika makaburi ya Mwanakwerekwe Mjini Zanzibar.(Picha na Ramadhan Othman IKULU)

Watoto wa marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu Adam Clement Mwakanjuki,wakiweka shada la mauwa katika kaburi wakati wa mazishi yake yaliyofanyika katika makaburi ya  Mwanakwerekwe Mjini Zanzibar. (Picha na Ramadhan Othman IKULU)

No comments:

Post a Comment