Msimamizi wa uchaguzi wa kura za maoni uliofanywa na wabunge kuwapata wagombea wa ubunge wa Afrika Mashariki kwa tiketi ya CCM, Abdulrahman Kianana akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa kikao cha uchaguzi huo, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, kwenye Ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam, leo. (Picha na Bashir Nkoromo)
Katibu wa Wabunge wa CCM, akimkaribisha Mwenyekiti wa wabunge wa CCM, Waziri Mkuu Mizengo Pinda kusimamia uchaguzi wa wagombea wa Ubunge wa Afrika Mashariki. Kulia ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye aliyekuwa msimamizi wa uchaguzi huo.
Wagombea wa kura za maoni wa ubunge wa Afrika Masharik,i wakinyoosha mikono kuunga mkonbo hoja wakati wa uchaguzi huo.
Wagombea wateule waliopita kwenye kura za maoni wa Bunge la Afrika Mashariki, Mwenyekiti wa Benki ya KCB, Dk. Edmund Mndolwa na Mbunge aliyemaliza kipindi kimoja cha ubunge wa bunge hilo, Dk. Said Gharib Bilal, wakijadili jambo, kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba, Dar es Salaam leo. Wateule wote wa kura za maoni katika uchaguzi wa kuwapata wagombea hao uliofanyika leo, waliitwa kwenye Ofisi hiyo ya CCM kwa hatua zaidi.
No comments:
Post a Comment