TANGAZO


Wednesday, April 4, 2012

maandalizi ya mkutano wa AFDB, mkoani Arusha

Waziri wa Fedha Mustafa Mkulo (katikati), akitoa ushauri leo, mjini Arusha kwa wajumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Maandalizi ya mkutano wa mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), juu ya hatua ambazo zinatakiwa kuchukuliwa ili kufanikisha maandalizi ya mkutano huo, ambao utafanyika mkoani Arusha kuanzia tarehe 28 mwezi Mei hadi Juni Mos,i mwaka huu. Mkutano huo utawashirikisha karibu wajumbe 3000, kutoka ndani ya nchi na nje ya nchi. (Picha na Tiganya Vincent- MAELEZO-Arusha)




Waziri wa Fedha Mustafa Mkulo (kushoto), Mkurugenzi Mtenadaji wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC), Elishilia Kaaya (kulia) na Mkuu wa Hazina Ndogo Arusha Rehema Mwakajube (katikati) wakibadilishana mawazo jana mjini Arusha mara baada ya  kupata taarifa na kujionea maendeleo ya ukarabati wa vyumba mbalimbali vitakavyotumika katika mkutano wa mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) ambao utafanyika mkoani Arusha kuanzia tarehe 28, mwezi Mei hadi Juni Mosi, mwaka huu. Mkutano huo utawashirikisha karibu wajumbe 3000, kutoka ndani ya nchi na nje ya nchi.





Waziri wa Fedha Mustafa Mkulo (kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magessa Mulongo (kushoto) wakibadilishana mawazo leo mjini Arusha, mara baada ya kumaliza kikao cha kuweka mikakati mbalimbali  mjini Arusha itakayosaidia kufanyika kwa  mkutano wa mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) ambao utafanyika mkoani humo.

 Waziri wa Fedha Mustafa Mkulo (kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magessa Mulongo (kulia) wakiweka mikakati mbalimbali leo, mjini Arusha, itakayosaidia kufanyika kwa  mkutano wa mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), ambao utafanyika mkoani Arusha kuanzia tarehe 28, mwezi Mei hadi Juni Mosi mwaka huu.



No comments:

Post a Comment