Mkurugenzi mpya wa Taasisi ya Vyombo Vya Habari, Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISA), Tumaini Mwailege akiwaeleza waandishi wa habari, umuhimu wa kupigania mazingira mazuri ya kazi na maslahi bora kazini, Dar es Salaam leo. Mwailege ameanza kazi rasmi leo 30/4/2012), amechukua nafasi ya Rose Haji, aliyemaliza muda wa utumishi wake katika taasisi hiyo, mwaka jana. Katikati ni Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Mohamed Tibanyendera na Mjumbe wa Bodi, Elias Mhegera. (Picha na Anna Nkinda - Maelezo)
Mkurugenzi mpya wa Taasisi ya Vyombo Vya Habari Kusini mwa Afrika Tawi la Tanzania (MISA), Tumaini Mwailege akifafanua jambo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu umuhimu wa kupigania mazingira mazuri na maslahi bora kazini. Katikati ni Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Mohamed Tibanyendera na Mjumbe wa Bodi, Elias Mhegera.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo Vya Habari Kusini mwa Afrika Tawi la Tanzania (MISA), Mohamed Tibanyendera, akijibu maswali ya waandishi wa habari, Dar es Salaam leo (hawapo pichani), kuhusiana na jinsi taasisi hiyo, inavyofanya kazi mbalimbali za kuhakikisha kuwa taaluma ya habari inaimarika hapa nchini. Kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Tumaini Mwailege.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo Vya Habari Kusini mwa Afrika Tawi la Tanzania (MISA), Mohamed Tibanyendera, akifafanua masuala mbalimbali kwa waandishi wa habari, wakati walizungumza nao, Dar es Salaam leo, wakati Mkurugenzi mpya wa Taasisi hiyo, Tumaini Mwailege (kulia), alipokuwa akijitambulisha. Kushoto ni mjumbe wa Bodi ya taasisi hiyo, Elias Mhegera.





No comments:
Post a Comment