TANGAZO


Thursday, April 19, 2012

Mkurugenzi Mkuu TPB, ashiriki kutoa huduma, Wiki ya Wateja


Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Sabasaba Moshingi, akibadilisha mawazo na Meneja Mwandamizi wa Mahusiano wa benki hiyo, Noves Moses, wakati alipofika kwenye tawi la Posta Mpya la benki hiyo, Dar es Salaam leo, kutoa huduma kwa wateja katika kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja wa TPB nchini. (Picha zote na Kassim Mbarouk)
 Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Sabasaba Moshingi (nyuma kushoto), akiwa pamoja na Meneja wa tawi la TPB, Posta Mpya, Nabwike Mwakajila (nyuma), wakati alipofika kwenye tawi hilo, kutoa huduma kwa wateja katika kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja wa benki hiyo leo. 



 Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Sabasaba Moshingi (kulia), akimkaribisha mteja wa benki hiyo, Mohamed Mkumbege, wakati alipofika kwenye tawi la Posta Mpya, jijini Dar es Salaam, kutoa huduma katika kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja wa TPB leo asubuhi.




 Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Sabasaba Moshingi (kushoto), akibadilishana mawazo na Meneja wa tawi la TPB, Posta Mpya, Nabwike Mwakajila (katikati) na Ofisa Huduma kwa  Wateja wa tawi hilo, Adolphina Maginga (kulia), wakati akiwa kwenye kaunta ya benki hiyo, kusubiri kutoa huduma kwa wateja.




Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Sabasaba Moshingi, akimhudumia mteja wa benki hiyo, Beatrice Lugenge (kushoto), kwenye tawi benki hiyo, la Posta Mpya leo asubuhi.




 Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Sabasaba Moshingi, akimsikiliza Ofisa Huduma kwa  Wateja wa tawi hilo, Adolphina Maginga (kushoto), wakati alipokuwa akitoa maelekezo kwa mteja wa tawi hilo la TPB, Leylat Msuri (kulia), wakati alipofika kupata huduma tawini hapo leo.




 Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Sabasaba Moshingi, akimkabidhi kadi mpya ya kutolea pesa kwenye ATM, inayojulikana kwa jina la Uhuru, mteja  ya benki hiyo, Leylat Msuri, baada ya kupatiwa maelekezo ya jinsi ya kutumia kadi hiyo, kutoka kwa Ofisa Huduma kwa  Wateja wa tawi hilo, Adolphina Maginga (kushoto), wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja. Wa pili kulia ni Meneja wa tawi la TPB, Posta Mpya, Nabwike Mwakajila.




 Mwandishi na mpigapicha wa Televisheni ya Chanel Ten, Khamis Suleiman (kushoto), akipatiwa maelezo na mmoja wa Maofisa wa TPB, tawi la Posta Mpya, wakati alipofika kwenye tawi hilo kupata huduma za kibenki, akiwa kama mteja wa TPB, leo asubuhi.




 Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Sabasaba Moshingi, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati alipokuwa kwenye tawi la TPB la Posta Mpya, kutoa huduma kwa wateja katika kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja. Kushoto ni Meneja wa tawi hilo, Nabwike Mwakajila.




Meneja wa benki ya Posta, tawi la Posta Mpya, Nabwike Mwakajila, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja tawini hapo. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Sabasaba Moshingi.

No comments:

Post a Comment