TANGAZO


Thursday, April 19, 2012

Wakimbizi wa Mali watorekea Mauritania

Wakimbizi wa Mali
Shirika la misaada la Medecins sans Frontieres, limesema kuwa idadi ya wakimbi wanaokimbilia Mauritania kutoka Kaskazini mwa Mali imeongezeka mara dufu.
Kwa mujibu wa shirika hilo, katika wiki mbili zilizopita , idadi yao imeongezeka kutoka watu mimbili hadi wakimbizi elfu moja miatano kila siku.
Wengi wa wakimbizi hao wana matatizo ya kiafya ikiwemo utapia mlo, huku hospitali ya karibu nao ikiwa umbali wa masaa sita kutoka kambini
Mwezi jana waasi waliteka sehemu kubwa za Kaskazini mwa Mali baada ya mapinduzi ya kijeshi kufanyika.
Ramani
Kulingana na shirika hilo wengi wa wakimbizi wanaoendelea kuwasili ni familia za kutoka jimbo la Timbuktu .
Wakati huoho, katibu mkuu wa umoja wa mataifa ametaka kuachiliwa kwa watu waliokamatwa baada ya kutekwa kwa eneo la putsch.
Wanajeshi waasi walikabidhi mamlaka kwa kiongozi wa kiraia wiki jana lakini baadhi ya washirika wa rais aliyengolewa mamlakani Amadou Toumani Toure, wamekamatwa tangu hapo.
Hata hivyo duru zinaarifu kuwa wanajeshi waliofanya mapinduzi hawana nia ya kuondoka kwenye siasa.
Mapinduzi ya mwezi jana nchini Mali, yalisababisha vurugu nchini M huku wapiganaji wa Tuareg kwa ushirikianao na wapigajai wa kiisilamu, waliteka sehemu kubwa ya Kaskazini mwa Mali.

No comments:

Post a Comment