TANGAZO


Saturday, April 28, 2012

Mdau wa Blogu ya Bayana achukua jiko

 Mdau wa Blogu ya Bayana, Hassan Twaha, mkazi wa Kagera, jijini Dar es Salaam, akifungishwa ndoa wakati alipokuwa akimuoa kimwana Haki Ally, mkazi wa Tabata Mawenzi jijini jana usiku. Aliyemshika mkono kumuozesha ni baba mzazi wa Haki, Ally Athuman Saidi. (Picha na Khamisi Mussa)




Kimwana Bi. Harusi, Haki Ally (kulia), akiwa amepozi kwa picha na mmoja wa dada zake wakati wa kufungwa ndoa hiyo.





Kimwana Bi. Harusi, Haki Ally, akiwa amepozi kwa picha wakati wa kufungwa ndoa hiyo.




Bi. Harusi, Haki Ally (wa pili kulia), akiwa amepozi kwa picha pamoja na ndugu zake wakati wa kufungwa ndoa hiyo.




Bi. Harusi, Haki Ally (katikati), akiwa na dada zake huku akitoa tabasamu la nguvu. 






Mdau Hassan Twaha, akiwa amemkumbatia mkewe, Bi. Haki Ally, mara baada ya kufungwa ndoa hiyo, Tabata Mawenzi jijini Dar es Salaam jana usiku.




Mdau Hassan Twaha, akipeana busu la nguvu na mkewe, Bi. Haki Ally, mara baada ya kufungwa ndoa hiyo na kukutanishwa kwenye chumba cha Bi. Harusi, Tabata Mawenzi jijini Dar es Salaam jana usiku.



Mdau Hassan Twaha na mkewe, Bi. Haki Ally, wakipozi kwa picha pamoja na dada za mkewe, wakati wa kupigwa picha za kumbukumbu ya harusi, chumbani kwa Bi. Harusi, Tabata Mawenzi jijini Dar es Salaam jana usiku.




Mdau Hassan Twaha na mkewe, Bi. Haki Ally pamoja na wasindikizaji wakiaga na kuondoka nyumbani kwao Bi. Harusi, Tabata Mawenzi, mara baada ya kumalizika sherehe za harusi hiyo, nyumbani hapo.

No comments:

Post a Comment