TANGAZO


Saturday, April 28, 2012

Kampuni ya DALBIT yakabidhi baiskeli kwa Taasisi ya MOI

 Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya Usambazaji Mafuta DALBIT, Magaret Mbaka, akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa ya Moi, Muhimbili,  Profesa Lawrance Museru, moja ya baiskeli 20, zilizotolewa na Kampuni hiyo kwa ajili ya kubebea wagonjwa, Hospitalini hapo jana. Mgonjwa aliyekaa kwenye baiskeli hiyo ni Gadson Gamason. (Picha zote na Khamisi Mussa)




 Mgonjwa aliyeketi kwenye baiskeli hiyo, Gadson Gamason, akizungumza na waandishi wa habari, baada ya kampuni ya DALBIT, kukabidhi baskeli hizo kwa taasisi hiyo.




 Baadhi ya baiskeli za wagonjwa zilizokabidhiwa kwa Taasisi ya Moi na Kampuni ya DALBIT.




 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa ya Moi, Muhimbili,  Profesa Lawrance Museru (kulia), akitoa shukurani kwa viongozi wa Kampuni ya DALBIT, kutokana na msaada huo.




 Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya Usambazaji Mafuta DALBIT, Magaret Mbaka, akisukuma baskeli iliyokuwa imembeba mgonjwa Gadson Gamason, mara baada ya kukabidhi baiskeli hizo kwa taasisi ya Moi, Muhimbili jijini Dar es Salaam jana.



 Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya Usambazaji Mafuta DALBIT, Magaret Mbaka na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa ya Moi, Muhimbili,  Profesa Lawrance Museru, wakiisukuma baskeli iliyombebea mgonjwa Gadson Gamason, wakati wa hafla ya makabidhiano hayo.




Uongozi wa Taasisi ya Mifupa ya Moi, ukiwa katika mazungumzo na Uongozi wa Kampuni ya DALBIT, mara baada ya makabidhiano ya msaada huo jana. 

No comments:

Post a Comment