Mama Salma Kikwete, akiwa amembeba mtoto Anna Julia Telles, mwenye umri wa miezi mitatu anayepata matibabu ya kansa katika Hospitali ya hiyo, mjini Brasilia nchini Brazili.
Mama Salma Kikwete, akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi wa Hospitali ya watoto wanaougua ugonjwa wa kansa, Marli Aparecide dos Santos, mara baada ya kumaliza ziara yake ya kutembelea hospitali hiyo, mjini Brasilia nchini Brazili leo.
Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete, akiangalia moja ya bidhaa zinazouzwa na Hospitali ya watoto wanaougua ugonjwa wa kansa kwa ajili ya kupata fedha za kuwasaidia watoto hao, huku Afisa ubalozi wa Tanzania nchini Brazili, Tabu Makata, akimuangalia. Hospitali hiyo, inatoa dawa aina ya chemotherapy kwa wagonjwa ambao ni watoto 500 kwa mwezi na hutibu asilimia sabini ya kansa.
Mama Salma Kikwete, akimsikiliza mmoja wa wafanyakazi wa Hospitali hiyo ya watoto waougua ugonjwa wa kansa, akielezea jinsi hospitali hiyo pamoja na jamii, inavyotoa huduma ya kujitolea kwa wagonjwa.
No comments:
Post a Comment