Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Ghariub Bilal,
akisikiliza maelezo kuhusu jinsi ya ufundishaji wanafunzi kwa kutumia mtambo wa kufua
Umeme, kutoka kwa Mwalimu wa Umeme Veta, Majolo Mwigole, wakati Makamu alipofika kuzindua Chuo cha VETA, mkoani Lindi jana Aprili, 10, 2012. (Picha na Muhidin Sufiani-OMR)
Umeme, kutoka kwa Mwalimu wa Umeme Veta, Majolo Mwigole, wakati Makamu alipofika kuzindua Chuo cha VETA, mkoani Lindi jana Aprili, 10, 2012. (Picha na Muhidin Sufiani-OMR)
Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Shukuru Kawambwa, Balozi wa Korea nchini, Young-Hoon Kim na Viongozi wa VETA, wakati akitembelea na kukagua baadhi ya majengo mapya yaliyojengwa ya Chuo cha Ufundi Stadi cha VETA, baada ya kukizindua rasmi chuo hicho, mkoani Lindi.
Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akibonyeza 'Alam', kuashiria uzinduzi rasmi wa Chuo kipya cha Ufundi Stadi cha VETA, kilichojengwa Mkoa wa Lindi. Uzinduzi huo ulifanyika jana.
Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal na Balozi wa Korea nchini, Young-Hoon Kim, wakikata utepe kwa pamoja kuashiria uzinduzi rasmi wa Chuo kipya cha Ufundi Stadi cha VETA, kilichojengwa mkoani Lindi. Uzinduzi huo ulifanyika jana, mkoani humo. Kulia ni Mkurugenzi wa VETA, Zebadia Moshi.
No comments:
Post a Comment