Lulua akiwa amepozi kwa picha |
MSANII wa filamu nchini Elizabeth
Michael maarufu kama 'Lulu' leo, asubuhi
amepandishwa kizimbani katika mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu kusomewa mashtakayake kufuatia kuhusika na kifo cha msanii mwenzake, Steven Charles Kanumba.
amepandishwa kizimbani katika mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu kusomewa mashtakayake kufuatia kuhusika na kifo cha msanii mwenzake, Steven Charles Kanumba.
Lulu amesomewa mashtaka hayo mbele ya hakimu Agustino Mmbando na wakili
Elizabeth Kaganda ya mauaji ya Kanumba yaliyotokea huko sinza Vatcan jijini Dar es Salaam aprili 7 mwaka huu.
Hata hivyo, mshtakiwa hakutakiwa kujibu chochote kwani mahakama hiyo haina mamlaka ya
kusikiliza kesi za mauaji ambapo kesi hiyo imeahirishwa tena na itaanza kusikilizwa tena aprili 23 mwaka huu.
Awali nyota huyo alifikishwa
mahakamani hapo chini ya ulinzi
mkali na kwa kasi ya ajabu hali iliyopelekea waandishi wa habari
kutopata wasaa hata wa kupiga picha, kabla ya kuondolewa mahakamani hapo
kwa gari aina ya Suzuki Grand Vitara yenye usajili namba T848 BNV na nambari za kwenye kioo PT 2565.
No comments:
Post a Comment