TANGAZO


Sunday, April 15, 2012

Kilimanjaro Music Award 2012, Diamond atwaa tuzo 3

Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Nassib Abdul, ‘Diamond' (kulia), akipokea tuzo yake kutoka kwa George Kavishe, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, mara baada ya kutangazwa mshindi wa utunzi bora wa nyimbo katika hafla ya kukabidhi tuzo kwa wanamuziki bora ya Kilimanjaro Music Award 2012, ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam jana usiku. Msanii Nassib Abdul ‘Diamond’ usiku wa kuamkia leo ameng’ara kwa kujinyakulia tuzo 3 za Kilimanjaro Music Award. Tuzo nyingine ni pamoja na ya Utunzi bora wa nyimbo na ya Video Bora ya Mwaka, kupitia wimbo wake wa Moyo Wangu, ambayo ilikuwa ya tatu kushinda.


Msanii Diamond akipiga picha pamoja na mama yake wa pili kushoto na Mkurugenzi wa ASET Asha Baraka (kulia) na wanenguaji wake.


Mwimbaji wa muziki wa Taarab, ambaye ameshinda tuzo ya mburudishaji bora kwa wanawake Malkia wa mipasho, Khadija Omar Kopa, akitumbuiza katika hafla hiyo usiku wa kuamkia leo.


Malkia Khadija Omar Kopa akishukuru wapenzi wake mara baada ya kushinda tuzo ya mburudishaji bora. Wa pili kushoto ni mume wake na wengine ni watoto wake.


Watoto wa Malkia wa Mipasho, Khadija Omar Kopa, wakishuka jukwaani mara baada ya kumtunza mama yao, wakati alipokuwa akitumbuiza katika hafla hiyo.


Msanii Profesa Jay (kulia) na Meneja wa kundi la TMK Family, Mkubwa Fella, wakimkabidhi tuzo Roma, msanii wa muziki wa Hip hop, aliyejishindia tuzo ya msanii bora wa Hip hop.


Wasanii wa kundi la Tanzania House of Talent (THT), wakionesha vipaji vyao katika hafla hiyo.
 

Wasanii wa kundi la Tanzania House of Talent (THT), wakiendela kumwaga burudani kwenye ukumbi huo.
 

No comments:

Post a Comment