TANGAZO


Sunday, April 15, 2012

Hafidhi apewa Wakfu wa Uaskofu Zanzibar

Askofu Michael Henry Hafidhi (mwenye vazi jekundu), akiwa amekaa muda mfupi kabla ya kutawazwa kuwa Askofu wa Anglican, Zanzibar leo. (Picha na Martin Kabemba)
 
 
 
Askofu mteule, Michael Henry Hafidhi (kulia) akila kiapo mbele ya Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglican Tanzania, Dk.Valentino Mokiwa. 

Maaskofu wa Anglican wa Tanzania, wakimwekea mikono, Askofu mteule, Michael Henry Hafidh wakati wa kumtawaza, mjini Zanzibar leo.

Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, akiwa ni mgeni rasmi akiwa pamoja na Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Benjamin William Mkapa, wakifuatilia Ibada ya kuwekwa Wakfu, Askofu Michael Henry Hafidhi, kwenye Kanisa la Anglican, Mkunazini mjini Zanzibar leo.
 
 
 
Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia kwenye Kanisa la Anglican, Mkunazini,  wakati wa Ibada ya kumweka wakfu, Askofu wa Anglican Zanzibar, Michael Henry Hafidh .


Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Awamu ya Tatu, Benjamin William Mkapa, akihutubia waumini wa Kikkristo na wageni waalikwa wakati wa Ibaada ya kuwekwa wakfu, Askofu wa Anglican Dayosisi ya Zanzibar, Michael Henry Hafidh, mjini Zanzibar leo.

No comments:

Post a Comment