TANGAZO


Sunday, April 15, 2012

Simba yaichapa Ruvu Shooting bao 1-0, Ligi ya Vodacom

 Michael Pius wa Ruvu Shootinga, akimtegea Emmanuel Okwi wa Simba wakati timu hizo zilipopambana katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. Simba imeshinda bao 1-0. (Picha zote na Kassim Mbarouk)


 Mchezaji Michael Pius wa Ruvu Shooting, akipiga mpira mbele ya Emmanuel Okwi wa Simba, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom kati ya timu hizo, uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.


  Gervais Kago wa Simba akimtoka Idd Nyambibo wa Ruvu katika mchezo huo.


  Amir Maftaha wa Simba, akitafuta mbinu ya kumtoka Michael Pius wa Ruvu Shooting.


 Mashabiki wa Simba, wakishangilia timu yao, baada ya kuichapa Ruvu Shooting bao 1-0, katika mchezo huo.


 Patrick Mafisango, akikimbia na kushangilia goli pekee aliloifungia timu yake dhidi ya Ruvu Shooting.


 Patrick Mafisango (kushoto) na Uhuru Suleiman wakishangilia pamoja goli hilo, lililoipa Simba poiti tatu na kupelekea kuendelea kuongoza ligi hiyo.


  Patrick Mafisango, akionesha namba ya jezi yake  kwa wapinzani wa timu yake (Yanga), baada ya kuifungia timu yake bao pekee katika mchezo huo dhidi ya Ruvu Shooting. Kulia  anayempongeza ni Amir Maftah wa timu hiyo.


Mchezaji Idd Nyambibo wa Ruvu Shooting, akimtoka Uhuru Suleiman wa Simba katika mchezo huo.

No comments:

Post a Comment