Mchungaji wa Usharika wa Kijitonyama, Ernest Kadiva (kushoto), akibadilishana mawazo na wajumbe wa kamati ya maandalizi ya uzinduzi wa jengo la Kijitonyama Lutheran Centre (KLC). Katikati ni Katibu wa Baraza la Kanisa hilo, Dk. Victoria Kayombe na Mzee wa Baraza la Kanisa, Leonard Shayo, wakati walipokutana na waandishi wa habari kwa ajili ya kutoa taarifa juu ya uzinduzi wa jengo hilo, utakaofanyika Jumapili ya tarehe 29 mwezi huu.
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Dayosisi ya Usharika wa Kijitonyama, Dk. Hans Macha (kulia), akisisitiza jambo kwa Katibu wa Kamati ya maandalizi ya uzinduzi wa jengo la Kijitonyama Lutheran Centre (KLC), Leonard Shayo, ambalo litatumika kama kitega uchumi cha kanisa hilo, baada ya kumaliza mkutano na waandishi wa habari kwa ajili ya kuwafahamisha juu ya uzinduzi wa jengo hilo.
Katibu wa Baraza la Kanisa hilo, Dk. Victoria Kayombe, akiongea na baadhi ya wanakamati ya maandalizi ya uzinduzi wa jengo la Kijitonyama Lutheran Centre (KLC), litakalotumika kama kitegauchumi cha kanisa hilo, mara baada ya kumaliza mkutano na waandishi wa habari juu ya uzinduzi wa jengo hilo, utakaofanyika Jumapili ya tarehe 29, mwezi huu. Wa pili kutoka kushoto ni Mchunga wa Usharika wa Kijitonyama, Ernest Kadiva, Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya uzinduzi Selina Mkony, Mzee wa baraza la kanisa Leonard Shayo na Mjumbe wa kamati hiyo, Peniel Uliwa. Ujenzi huo umegharimu kiasi cha Bilioni 3.5
Katibu wa baraza la Kanisa hilo Dk. Victoria Kayombe, akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na maandalizi ya uzinduzi wa Jengo la Kijitonya Lutheran Centre (KLC), litakalotumika kama kitegauchumi cha Kanisa hilo, Jengo hilo litazinduliwa rasmi, Aprili 29. Katikati ni Mchungaji wa Usharika wa Kijitonyama Ernest Kadiva na Mwenyekiti wa ujenzi, Sanyiel Kishimbo.
Baadhi ya waumini na wanakamati wa maandalizi ya uzinduzi wa jengo la Kijitonyama Lutheran Centre (KLC), walioudhuria kwenye mkutano na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya uzinduzi wa jengo hilo litakalozinduliwa Jumapili ya tarehe 29 mwezi huu, wakisikiliza maelezo mbalimbali yaliyokuwa yakitolewa kwa waandishi.
No comments:
Post a Comment