TANGAZO


Friday, April 6, 2012

Ibada ya Ijumaa Kuu St. Joseph mjini Zanzibar

Askofu wa Kanisa Katoliki, jimbo la Zanzibar, Mhashamu Augustino Shao, akitoa ujumbe wa Ijumaa Kuu, mjini Zanzibar leo, ambapo ameagiza vyombo husika kushughulikia mateso ya watu wanaoteseka bila hatia, akitolea mfano wa watu walioko rumande kwa muda mrefu bila kufikishwa Mahakamani. (Picha na Martin Kabemba)


Waumini wakisikiliza ujumbe kutoka kwa Askofu wa Kanisa Katoliki jimbo la Zanzibar, Mhashamu Augustino Shao, wakati wa Ibada ya Ijumaa Kuu kwenye Kanisa la St. Joseph mjini Zanzibar  leo jioni.



Padri Cosmas Aman Shayo, akionesha msalaba wa Yesu kwa waumini waliohudhuria Ibada ya Ijumaa Kuu tayari kuanza kuabudu kwa kuubusu kwenye kanisa hilo leo jioni.



Padri Thomas Assenga wa Kanisa la St. Joseph mjini zanzibar, akibusu msalaba wakati wa kuadhimisha Ibada ya Ijumaa Kuu, mjini zanzibar leo. 

No comments:

Post a Comment