TANGAZO


Friday, April 6, 2012

Dk. Bilal, azungumza na wanamichezo wa Ikulu za Dar na Zanzibar

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na wanamichezo wa Ikulu, wakati akiwaaga na kuwatakia ushindi wakienda kushiriki katika bonanza maalum la Pasaka, linaloanza leo, Aprili 06, 2012, Viwanja vya Sigara (TCC Chang’ombe), Dar es Salaam. Makamu alikutana na wanamichezo hao,  Ikulu ya Zanzibar na Dar es Salaam leo asubuhi. (Picha na Muhidin Sufiani-OMR)

Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na wanamichezo hao Ikulu, wakati akiwaaga na kuwatakia ushindi kuelekea kushiriki katika Bonanza maalum la Pasaka linaloanza leo, Viwanja vya Sigara, Chang’ombe, jijini Dar es Salaam. Makamu alikutana na wanamichezo hao wa Ikulu ya Zanzibar na Dar es Salaam, leo asubuhi Ikulu ya jijini. Kulia ni Katibu Mkuu wa Ikulu, Peter  Ilomo na kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Mwinyiusi Hassan.  





Baadhi ya wanamichezo, wafanyakazi wa Ikulu, wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, wakati akizungumza nao, akiwatakiwa mafanikio na ushindi kwenye bonanza hilo maalum la Pasaka linaloanza leo jijini Dar es Salaam. 




Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya Wafanyakazi  na wanamichezo hao wa kulu ya Dar es Salaam na Zanzibar, baada ya kumaliza mazungumzo nao, Ikulu jijini.




Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi ‘wanamichezo’ wa Ikulu za Zanzibar na Dar es Salaam, leo jijini.

No comments:

Post a Comment