TANGAZO


Friday, April 6, 2012

Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania yazinduliwa


 Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Bodi mpya ya Wakurugenzi ya Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), iliyozinduliwa jana, Makao Makuu ya Wizara ya Maliasili, Jengo la Mpingo, Keko jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Balozi Charles Sanga na Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii (TTB), Dk. Aloyce Nzuki. (Picha na Mpigapicha wetu)

Mwenyeikiti wa Bodi ya Utalii ya TTB, Balozi Charles Sanga,  akizungumza katika uzinduzi bodi hiyo. Wanaofuatia katika picha ni Mkurugenzi wa TTB, Dk. Aloyce Nzuki na wajumbe wa bodi, Abdulkarim Shah, Kaika Telele na Isaya Jairo.


Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Maimuna Tarishi, akizungumza, wakati akimkaribisha Waziri wa Maliasili Ezekiel Maige (kushoto), ili kuzungumza katika uzinduzi huo. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Ibarahim Mussa.


Baadhi ya Wakurugenzi wa vitengo mbalimbali vya Wizara ya Maliasili na Utalii, wakiwa katika uzinduzi huo.


Meneja wa Masoko wa Bodi ya Utalii, Geofrey Meena (kushoto), akiwa na wakuu wengine wa vitengo katika bodi hiyo ya Utalii TTB.


Wakuu wa vitengo mbalimbali kutoka bodi ya Utalii TTB, wakiwa kwenye uzinduzi huo.


Wajumbe wa Bodi ya Utalii ya TTB, wakiwa katika uzinduzi huo. Kutoka kushoto ni Teddy Mapunda, Isaya Jairo, Kaika Telele, Abdulkarim Shah na Mkurugenzi wa TTB, Dk. Aloyce Nzuki.


Mjumbe  wa Bodi ya Utalii ya TTB, Teddy Mapunda, akijitambulisha kwenye uzinduzi huo. Wengine ni wajumbe wenzake wa bodi hiyo.


Baadhi ya Maofisa wa Bodi ya Utalii, wakifuatilia uzinduzi huo jana.

.
Waziri Ezekiel Maige (katikati), akiwa pamoja na Wakurugenzi wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Bodi ya Wakurugenzi ya TTB pamoja na Maofisa wa TTB.


Waziri Ezekiel Maige (katikati), akiwa  katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara pamoja na Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Utalii Tanzania.


Waziri Ezekiel Maige (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara, Maimuna Tarishi (wa tatu kushoto), Naibu Katibu Mkuu, Nuru Millao (wa pili kulia) na baadhi ya Wakurugenzi wa Idara mbalimbali za Wizara hiyo.

No comments:

Post a Comment