TANGAZO


Friday, April 6, 2012

Rais Kikwete, akitangaza wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba

Rais Jakaya Kikwete, akitangaza majina ya wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dar es Salaam leo. Wanaoshuhudia ni Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Iddi na Waziri wa Sheria na Katiba, Celina Kombani. (Picha na Ikulu)






Baadhi ya Wahariri wa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam, wakimsubiri Rais Kikwete, kutangaza majina ya wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba leo, Ikulu jijini Dar es Salaam.




Rais Kikwete akiwa na Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilali, wakitoka kwenye chumba cha mikutano Ikulu, baada ya Rais kutangaza Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba.


Rais Kikwete akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari Ikulu jijini leo, kuhusu Tume ya Mabadiliko ya Katiba aliyoitangaza. Rais alisisitiza kwamba tarehe ya kuanza kazi itatangazwa rasmi mara baada ya wajumbe wote kujulishwa uteuzi wao na baadaye kuapishwa. Alifafanua kuwa kisheria, Tume inatakiwa iwe imekamilisha kazi ndani ya miezi 18.



No comments:

Post a Comment