TANGAZO


Saturday, April 7, 2012

Hitima ya kumbukumbu ya kifo cha Karume

Rais wa Zanzibar na  Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein,(katikati)  Rais wa mstaafu wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi,(wa pili kushoto) akimuakilisha, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete,Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji,na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Omar Qaabi,pamoja na viongozi wengine wakisoma hitmaya kumuombea dua Muasisi wa Mapinduzi,na Rais wa Kwanza wa Zanzibar Abeid Amani Karume, Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]


Baadhi ya Mabalozi na Wananchi waliohudhuria katika kisomo
cha dua ya kumuombea marehemu Rais wa Kwanza wa Zanzibar Mzee Abeid
Amani Karume,huko Ukumbi wa CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar  leo.[Picha
na Ramadhan Othman,Ikulu.]

Mke wa Muasisi wa Mapinduzi na Rais wa kwanza wa Zanzibar, Mama Fatma Karume,(wa nne kushoto) pamoja na wake wa Viongozi mbalimbali wakiwa katika hitma ya kumuombea dua Marehemu Mzee Abeid Amani Karume,huko Ukumbi wa CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar leo.


Baadhi ya Akina mama wa Mitaa mbali mbali ya Unguja, wakimuombea Dua marehemu Mzee Abeid Amani Karume,huko Ukumbi wa CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar leo.




Rais wa Zanzibar  na  Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein,a kiweka Shada la mauwa katika kaburi la Muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar Mzee Abeid Amani Karume leo viwanja vya CCM Kisiwandui mjini Unguja.
 

Viongozi wa Kitaifa wakimuombea dua Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume,katika kaburi alipozikwa kiongozi huyo huko Viwanja vya CCM KIsiwandui Mjini Zanzibar leo asubuhi.


Mke wa Muasisi wa Mapinduzi na Rais wa kwanza wa Zanzibar , Mama Fatma Karume,(kushoto) pamoja na wake wa Viongozi mbalimbali, wakiomba dua katika kaburi la Marehemu Mzee Abeid Amani
Karume, huko viwanja vya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar leo.

No comments:

Post a Comment