TANGAZO


Saturday, April 7, 2012

Kikwete atoa msaada wa Pasaka

Katibu tawala mkoa wa Singida,Liana Hassan,akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi zawadi zilizotolewa na rais Jakaya Kikwete,kwa wakazi wa kambi ya Sukamahela,wilayani Manyoni juzi.Kushoto ni mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Manyoni,Fotunata Malya na anayefuata,ni mke wa Ras,Liana Hassani. (Picha zote na Nathaniel Limu)


Katibu tawala mkoa wa Singida,(kulia) akikabidhi mbuzi watatu wakiwa ni zawadi kutoka kwa rais Kikwete kwa wazee wasiojiweza wa kambi ya Sukamahela wilayani Manyoni jana.


Katibu Tawala mkoa wa Singida,Liana Hassan (kulia) akikabidhi dumu la mafuta ya alizeti moja ya zawadi zilizotolewa na Rais Kikwete kwa wakazi wa kambi ya wazee ya Sukamahela.



Katibu tawala mkoa wa Singida, Liana Hassan,(kulia) akimvisha shati mmoja wa wakazi wa kambi ya wazee ya Sukamahela.

,Mkazi wa kambi ya wazee wasiojiweza ya Sukamahela wilayani Manyoni,Kareudia Madoli,akitoa shukurani kwa niaba ya wenzake kwa rais Kikwete kwa msaada wake kwa ajili ya sherehe ya pasaka.

No comments:

Post a Comment