TANGAZO


Monday, April 16, 2012

Dk. Bilal azindua benki ya ABC, mjini Arusha

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake ya ufunguzi, wakati alipokuwa akizindua rasmi jengo la Benki ya ABC jijini Arusha leo Aprili 16, 2012. (Picha na Muhidin Sufiani-OMR)

Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal na Mwenyekiti wa bodi wa benki ya ABC ya jijini Arusha, Dk. Jonas Kipokola, wakifunua kitambaa kuashiria kuweka jiwe la msingi la benki hiyo, wakati Makamu alipofika jijini humo, kuizindua rasmi, jijini humo.

Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal na Mwenyekiti wa bodi wa benki ya ABC ya jijini Arusha, Dk. Jonas Kipokola, wakifurahia baada ya kuizindua rasmi na kuweka jiwe la msingi la benki hiyo mpya.


Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa benki ya ABC tawi la Arusha, Anna Kavishe, kuhusu masuala ya utendaji kazi na ramani ya jengo jipya la benki hiyo, baada ya kuizindua. Wapili kulia ni mke wake, Mama Zakhia Bilal na Kulia kwa Makamu ni Mwenyekiti wa bodi ya benki hiyo, Jonas Kipokola.


Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na viongozi pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo, mara baada ya kuizindua jana. Wapili kushoto ni mke wake, Mama Zakhia Bilal na kushoto kwa Makamu ni Mwenyekiti wa bodi ya benki hiyo, Jonas Kipokola.

No comments:

Post a Comment