Monday, April 16, 2012
Rais Kikwete awasili Brazil kwa ziara ya siku 5
Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete, akipokea shada la maua kutoka kwa Benny Queiroz, ikiwa ni ishara ya kumkaribisha mjini Sau Paul, nchini Brazil. Katikati ni Mumewe, Rais Jakaya Mrisho Kikwete. Rais na ujumbe wake wamo nchini humo kwa ziara ya kikazi ya siku 5. (Picha na Anna Nkinda - Maelezo)
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji (TIC), Raymond Mbilinyi, baada ya kuwasili Jumapili Aprili 15, 2012 katika hoteli ya Tivoli jijini Sao Paulo, Brazil, tayari kwa ziara ya siku tano ya kikazi nchini humo. (Picha na Ikulu)
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono mwandishi mwandamizi wa Habari Leo na Daily News, Joseph Lugendo, alipokuwa analakiwa baada ya kuwasilii Jumapili Aprili 15, 2012 katika hoteli ya Tivoli jijini Sao Paulo, Brazil, tayari kwa ziara hiyo.
Rais Jakaya Mrisho kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwasili hoteli ya Tivoli jijini Sao Paulo, Brazil, tayari kwa ziara ya siku tano ya kikazi nchini humo. Kulia ni Waziri wa kazi na Uwezeshaji Wanachi Kiuchumi na Ushirika wa Zanzibar, Haroun Ali Suleiman.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment