TANGAZO


Wednesday, April 25, 2012

Bilal awa mgeni rasmi maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal,
akisoma hotuba yake, wakati wa Kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Malaria
Duniani, zilizofanyika leo Aprili 25, 2012, Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Katika sherehe hizo pia Makamu wa Rais alizindua Ripoti ya Utekelezaji wa Mikakati ya Malaria Tanzania Bara. (Picha na Muhidin Sufiani-OMR)


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal,
akikata utepe, kuzindua Ripoti ya Mafanikio ya Utekelezaji wa Mikakati ya Malaria kwa
upande wa Tanzania Bara, wakati wa sherehe za maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Malaria
Duniani zilizofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo. Katikati ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Haji Mponda. Wa pili kushoto ni Kaimu Mkuu wa Wilaya za Kinondoni, Temeke na Ilala, Jordan Rugimbana. 


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal (wa pili kulia) na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Haji Mponda (wa tatu), wakipia makofi huku Kaimu Mkuu wa Wilaya za Kinondoni, Temeke na Ilala, Jordan Rugimbana (wa tatu kushoto), na viongozi wengine waliokuwepo meza kuu, wakikinyanyua juu kitabu cha Ripoti ya Mafanikio ya Utekelezaji wa Mikakati ya Malaria kwa upande wa Tanzania Bara, wakati wa sherehe za maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Malaria Duniani, zilizofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment