TANGAZO


Tuesday, April 24, 2012

Kiir,''Sudan imetangaza vita dhidi yetu''

Soko lililoshambuliwa Sudan Kusini
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir amesema Jamuhuri ya Sudan imetangaza vita dhidi ya nchi yake kufuatia mapigano katika mpaka baina ya nchi mbili.
Bw Kiir alisema haya wakati akiwa katika ziara rasmi nchini China ambayo ni mteja mkuu wa matufa kutoka nchi hizo.Huku haya yakiarifiwa, ndege za kijeshi za Sudan zimeendelea kudodosha mabomu kwenye maeneo ya mpaka mapema leo asubuhi.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amelaani mashambulio hayo ambapo mtu mmoja ameuawa na wengi kujeruhiwa.
Mashambulio ya karibuni yametokea katika miji ya Panakwatch,Lalop na kituo cha mpakani cha Teshwin. Sudan Kusini ilipata uhuru wake mwaka jana kufuatia vita vya zaidi ya miongo miwili.
Hata hivyo taharuki imeendelea kati ya pande mbili hususan tofauti dhidi ya raslimali za mafuta pamoja na mipaka kamili ya maeneo hayo.
Matamshi ya rais Kiir yametokea wakati akikutana na mwenzake wa China Hu Jintao mjini Beijing ambapo anafanya ziara ya siku tano.
Kiongozi huyo ametaja ziara yake kama muhimu akisema kwa maneno yake,''wakati jirani wetu Sudan ametangaza vita dhidi ya Sudan Kusini''.
Kwa upande wake Rais wa China Hu Jintao ametaka pande zote kujizuia na vitendo vya kuhujumu usalama.
Japo Sudan haijatangaza vita, wadadisi wanasema matamshi ya rais Omar Al bashir ya karibuni yanazua wasi wasi kuhusu kuendelea kwa mapigano.
Rais Bashir amesema hakuna uwezekano wa kufanya mazungumzo na Sudan Kusini na kuapa kuendelea na harakati za kijeshi hadi pale wanajeshi wa Sudan Kusini na washirika wao waondoke kutoka arthi ya Sudan.

No comments:

Post a Comment