TANGAZO


Thursday, April 12, 2012

Benki ya Posta yafungua tawi Ilala Boma

 Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Posta Tanzania (TPB), Sabasaba Moshingi, akikata utepe kuashiria ufunguzi wa tawi jipya la benki hiyo, lililopo kwenye jengo la Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ilala jijini Dar es Salaam leo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Majanga, Moses Manyatta na Meneja wa tawi hilo, Salma Marijani na kulia ni Meneja Uhusiano wa TPB, Noves Moses. (Picha na Kassim Mbarouk)




Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Posta nchini (TPB), Sabasaba Moshingi, akiongea na 
na wateja wa benki hiyo tawi la Ilala wakati alipokuwa akilifungua tawi hilo.




Meneja wa benki ya Posta tawi la Ilala, Salma Marijani, akiongea na
wateja wake, wakati wa ufunguzi wa tawi hilo leo asubuhi.



Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Posta nchini (TPB), Sabasaba Moshingi, akimsalimia mmoja wa wateja wa tawi hilo, mara baada ya kulifungua tawi jipya la benki hiyo, Ilala Boma, jijini Dar es Salaam.

 


Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Posta Tanzania (TPB), Sabasaba Moshingi, akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa ngazi mbalimbali na wafanyakazi wa tawi la Ilala, mara baada ya kulifungua.

No comments:

Post a Comment