Balozi wa Indonesia nchini Tanzania, Yudhistiranto Sungadi (kushoto), akimkabidhi Diwani wa Wadi ya Kikwajuni, Mahboub Juma Issa, miche ya minazi iliyotolewa na ubalozi wake kwa jumuia ya Imarisha Mazingira Zanzibar (JIMZ), ambapo inategemewa kupandwa katika eneo la Kizingi, mjini Zanzibar.(Picha zote na Haroub Hussein)
Balozi wa Indonesia nchini Tanzania, Yudhistiranto Sungadi (kushoto), akipanda mnazi
kuashiria uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti katika eneo la Kizingo, mjini Zanzibar leo, ambapo miti ipatayo 3,000, inategemewa kupandwa katikazoezi hilo linalofanywa na Jumuia ya Imarisha Mazingira Zanzibar (JIMZ) ya Kikwajuni. Kulia ni Katibu wa Jumuia hiyo, Rajab Ali na Diwani wa wadi ya Kikwajuni, Mahboub Juma Issa.
Balozi wa Indonesia nchini Tanzania, Yudhistiranto Sungadi (kushoto), akipanda mnazi
kuashiria uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti katika eneo la Kizingo, mjini Zanzibar leo, akisaidiwa na Katibu wa Jumuia hiyo, Rajab Ali (kilia) na Diwani wa wadi ya Kikwajuni, Mahboub Juma Issa.
No comments:
Post a Comment