Sunday, April 1, 2012
Airtel yawakutanisha watoto wa wafanyakazi na wateja kuelekea Siku Kuu ya Pasaka
Watoto wa wateja wa kampuni ya Airtel Tanzania wakijumuika kwa pamoja na watoto wa wafanyakazi wa Airtel kukakata keki iliyoandaliwa na kampuni ya Airtel Tanzania katika shamra shamra za tamasha maalum, kuelekea Siku Kuu ya Pasaka ambapo watoto hao walipata nafasi ya kucheza michezo mbalimbali kwa pamoja, iliyofanyika kituo cha michezo ya watoto kiitwacho Fun Sport ndani ya jengo la Qualty center, jijini Dar-es-salaam leo. (Picha na Mpigapicha Wetu)
Watoto wa wateja wa Kampuni ya Airtel Tanzania watoto wa wafanyakazi wa Airtel wakiwa katika shamra shamra za tamasha maalum la watoto kuelekea kusheherekea sikukuu ya pasaka katika kituo cha michezo ya watoto kiitwacho Fun Sport, Qualty center jijini Dar-es-Salaam kwa hisani ya Airtel.
Meneja mauzo wa Kampuni ya Airtel Tanzania, .Hilda Nakajumo akikata keki kwa pamoja na watoto wa wateja wa kampuni ya Airtel Tanzania na wa wafanyakazi katika shamra shamra za kuelekea Sikukuu ya Pasaka, ambapo watoto hao walipata nafasi ya kucheza michezo mbalimbali kwa pamoja ambayo katika kituo cha michezo hicho.
Mkurugenzi wa Biashara wa Kampuni ya Airtel Tanzania, Irene Madeje akizungumza na waandishi wa habari katika sherehe ya michezo kwa watoto wa wateja wa kampuni ya Airtel Tanzania na wa wafanyakazi wa kampuni hiyo katika shamra shamra za kuelekea Sikukuu ya Pasaka na kuendeleza uhusiano mzuri uliopo kati ya wateja na wafanyakazi wa Airtel.
Watoto wakicheza mchezo wa kuendesha magari wakati wa tamasha maalum la michezo kwa watoto lilioandaliwa na Airtel ili kutoa nafasi kwa watoto wafanyakazi wa Airtel pamoja na wa wateja kukutana na kucheza michezo mbalimbali pamoja kwa ajili ya tamasha shamra shamra ya kusherehekea Sikukuu ya Pasaka.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment