TANGAZO


Sunday, April 1, 2012

Vodacom foundation yatoa mikopo isiyo na riba kwa wajasiriamali, Mlandizi kupitia mradi wa mwei


Meneja wa mradi wa MWEI, unaondeshwa na Vodacom Tanzania, Mwamvua Mlangwa, akimkabidhi Fedha, Radhia Abdallah, ambazo ni mkopo usio na riba uliotolewa na Kampuni hiyo, ambao utarudishwa kwa njia ya m-pesa.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza, akimkabidhi fedha Mwanaidi Said, ambaye ni mmoja wa akinamama wajasiriamali wa kikundi cha Kilangalanga cha Mlandizi mkoani humo. Fedha hizo zilitolewa na Vodacom Tanzania kupitia mradi wake wa MWEI kwa ajili ya kusaidia wakinamama wajasiriamali.




Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza, akimkabidhi fedha Khadija Khalifan, ambaye ni mmoja wa akinamama wajasiliamali wa kikundi hicho, zilizotolewa na Vodacom kupitia mradi wake wa MWEI kwa ajili ya kusaidia wakinamama wajasiriamali. Katikati ni Meneja mradi huo, Mwamvua Mlangwa na Kuliani Diwani wa kata ya Janga Mlandizi, Fedilia Simba.
Baadhi ya akina mama wajasiriamali wa kikundi cha Kilangalanga kilichopo Mlanzidi mkoani Pwani, wakifurahia kupata mikopo isiyo na riba kutoka Vodacom Tanzania kupitia mradi wake wa MWEI. Jumla ya kinamama 425 wamenufaika na mkopo huo wa zaidi ya shilingi mil. 30.

No comments:

Post a Comment