TANGAZO


Wednesday, March 14, 2012

Yanga yaitwanga African Lyon FC bao 1 - 0

 Mchezaji Keneth Asamoah wa Yanga akimtoka Khamis Yussuf wa African Lyon FC, wakati timu zao zilipopambana katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo jioni. Yanga ilishinda bao 1-0. (Picha na Kassim Mbarouk)




Idriss Senga (kulia) wa Yanga, akiruka kwanja la Sino Augustino wa African Lyon katika mchezo huo.




 Pius Hendry wa Yanga, akiwa ameanguka chini wakati akizuia mpira huku akizongwa na Salamusasa Obina wa African Lyon.




 Golikipa Abdul Seif, akidaka mpira mbele ya mshambuliaji Keneth Asamoah wa Yanga.





Mchezaji Shamte Ally wa Yanga, akipambana na Sunday Bakari wa African Lyon, anayepiga tik tak, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo jioni.







 Shadrack Nsajigwa akitafuta mbinu ya kumtoka Khamis Yussuf wa African Lyon katika mchezo huo.


 Mashabiki wa African Lyon, wakiwapungia wachezaji wao, wakati wa kuingia Uwanjani kuanza kipindi cha pili cha mchezo huo.


Mashabiki wa Yanga, wakifuatilia mchezo huo, wakati wa kipindi cha pili cha mtanange huo.

No comments:

Post a Comment