Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad, akimsikiliza Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa Zanzibar Dk. Amina, akitoa maelezo ya jengo la Makumbusho ya Taifa la Bet el Aljaib Forodhani. (Picha na Mpigapicha Wetu)
Msimamizi wa Ujenzi Mansoor Rashid, akitoa maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa Makumbusho ya Taifa Mnazi mmoja, unaofanywa na Kampuni ya Lucky Construction Ltd , wakati wa ziara ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad alipotembelea jengo hilo na kuona maendeleo yake leo asubuhi.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad, akiangalia vitu vya zamani vilivyohifadhiwa katika Makumbusho ya Taifa Mnazi Mmoja, mjini Zanzibar wakati wa ziara yake leo.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, akimsikiliza mfanyakazi wa Makumbusho ya Taifa katika jengo la Mnazi Mmoja, Mwalimu Khamis, alipofika kujionea historia ya Zanzibar, iliyohifadhiwa katika makumbosho hiyo.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad, akipata maelezo ya Magofu ya Mtoni katika kitabu kinachoelezea historia ya magofu hayo, kutoka kwa Meneja wa Hoteli ya Mtoni Marine, Tonino Garav, akiwa katika ziara ya kutembelea majengo ya historia ya Zanzibar.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad, akimsikiliza Meneja wa Kampuni ya Ujenzi ya Lucky Construction Ltd, Ali Said Seif, wakati alipokuwa akitoa maelezo ya ujenzi huo unaofanywa na Kampuni yake.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad, akitembelea Magofu ya Mtoni kuangalia uendelezwaji wake kwa matumizi ya Historia ya Zanzibar kwa faida ya vizazi vijavyo na vivutio vya Utalii wa Zanzibar.
No comments:
Post a Comment