TANGAZO

Wednesday, March 14, 2012

Rais Kikwete afungua mkutano wa Chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimshukuru Rais wa chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno Nchini Dk. Rachel Mhavile baada ya kumkabidhi tuzo kutokana na juhudi zake za kuhamasisha masuala ya kinywa na meno ndani na nje ya nchi . Rais Kikwete alikuwa mgeni rasmi katika mkutano wa siku tatu wa kujadili jinsi ya kuyaweka masuala ya kinywa na meno katika hatua ya awali ya kupata huduma ambapo jumla ya wajumbe kutoka nchi 18 wanahudhuria mkutano huo. (Picha na Anna Nkinda - Maelezo)

Baadhi ya wajumbe wanahudhuria mkutano wa siku tatu wa kujadili jinsi ya kuyaweka masuala ya kinywa na meno katika hatua ya awali ya kupata huduma wakimsikiliza Rais Jakaya Mrisho Kikwete (hayupo pichani) wakati akifungua mkutano huo. Jumla ya wajumbe kutoka nchi 18 wanahudhuria mkutano huo unaofanyika jijini Dar es Salaam.

Madaktari wa Kinywa na Meno wakiwa katika picha ya pamoja na Rais Jakaya Kikwete, mara baada ya kuufungua Mkutano wao leo jijini Dar es Salaam.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Rais wa chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno Nchini Dk. Rachel Mhavile (kushoto) na Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali Dk. Donnan Mmbando baada ya kufungua mkutano wa siku tatu wa kujadili jinsi ya kuyaweka masuala ya kinywa na meno katika hatua ya awali ya kupata huduma ambapo jumla ya wajumbe kutoka nchi 18 wanahudhuria mkutano huo.

No comments:

Post a Comment