Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya maandalizi ya tuzo kwa waandishi wa habari, wakiwa katika kikao cha mwisho ya kukamilisha matayarisho ya tuzo hiyo, Makao Makuu ya Baraza la Habari Tanzania (MCT), Mwenge jijini Dar es Salaam leo.
Wajumbe wa Kamati ya Tuzo kwa waandishi wa habari, Alan Lawa na Fauzia Isamail Aboud, wakisikiliza mjadala katika kikao chao cha matayarisho ya mwsho ya tuzo hizo, Makao Makuu ya Baraza hilo, Mwenge jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
Katibu Mtendaji wa MCT, Kajubi Mukajanga, akizungumza na wajumbe wa kamati ya maandalizi ya tuzo za waandishi wa habari (EJAT) itakayofanyika hivi karibuni, pamoja na waandishi wa habari wakati akishukuru Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) kufuatia msaada wa shilingi milioni 10.925.000 ilioutoa kwa baraza hilo kwa ajili ya maandalizi ya tuzo hizo, katika mkutano uliofanyika kwenye makao makuu ya baraza hilo Mwenge jijini Dar es salaam, katika picha katikati ni Teddy Mapunda Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) na kushoto ni Mwenyekiti wa Jukwa la Wahariri Absalom Kibanda.
Mwenyekiti wa Jukwa la Wahariri, Absalom Kibanda, akizungumza wakati wa hafla ya Serengeti Bia, kukabidhi hundi ya sh. milioni 10, 925,000 kwa Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwa ajili ya kufanikisha kutoa tuzo kwa waandishi wa habari. Katikati ni Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), Teddy Mapunda na kushoto ni Katibu Mtendaji wa MCT, Kajubi Mukajanga.
Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), Teddy Mapunda, akizungumza kuhusu msaada wao kwa Baraza la Habari Tanzania katika kufanikisha tuzo za waandishi katika mkutano wa kupanga mikakati ya mwisho ya kutoa tuzo hizo, Dar es Salaam leo asubuhi. Kulia ni Mwenyekiti wa Jukwa la Wahariri, Absalom Kibanda, waliofanikisha kupatikana kwa ufadhili wa kampuni hiyo.
Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), Teddy Mapunda, akizungumza kuhusu msaada wao kwa Baraza la Habari Tanzania katika kufanikisha tuzo za waandishi katika mkutano wa kupanga mikakati ya mwisho ya kutoa tuzo hizo, Dar es Salaam leo asubuhi. Kulia ni Mwenyekiti wa Jukwa la Wahariri, Absalom Kibanda, ambalo limesaidia katika kupatikana kwa ufadhili huo na kushoto ni Katibu Mtendaji wa MCT, Kajubi Mukajanga.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda na Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), Teddy Mapunda, wakikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 10, 925,000 kwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) , Kajubi Mukajanga, fedha ambazo Kampuni ya (SBL) imetoa kwa Baraza hilo kwa ajili ya kufanikisha tuzo hizo. Kushoto ni Meneja Miradi ya jamii wa kampuni hiyo, Nandi Mwiyombella.
No comments:
Post a Comment