TANGAZO


Monday, March 19, 2012

Wizara ya Habari Zanzibar yatakiwa kutoa motisha kwa wafanyakazi





Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamadi



Na Maelezo Zanzibar  

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad amewataka viongozi wa Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo kutoa motisha kwa wafanya kazi wao sambamba na kuboresha vitendea kazi ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi.
Amesema suala la kuwapa motisha wafanya kazi wanaofanya majukumu yao vizuri huchochea ari  jambo ambalo hupelekea wafanya kazi wengine kuiga mfano huo na hivyo ufanisi kupatikana 
Maalim Seif ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na wafanyakazi wa Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo katika ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Zanzibar ili kujua maoni yao juu ya utendaji kazi wao wa kila siku
Amesema ni vyema maoni yaliyotolewa na wafanyakazi hao yakapatiwa majibu ya kueleweka ikiwa ni pamoja na kuhakikisha changamoto ndogo ndogo zinazowakabili wafanya kazi zinatatuliwa katika muda unaofaa.
Amesema katika kukabiliana na kasi ya ukuaji wa teknologia ni vyema kila Idara kuhakikisha kuwa inaanzisha programu za mafunzo kwa wafanyakazi wao ili kuwafanya wawe wa kisasa na kuhimili ushindani
Akizungumzia kuhusu mabadiliko ya mfumo wa Teknolojia kutoka Analogia kwenda Dijitali ambao unaanza mwishoni mwa mwaka huu katika ukanda wa Afrika ya Mashariki Maalim Seif amesema lazima kuhakikisha wafanyazi wa Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC wanapatiwa utaalamu wa kutosha ili kwenda sambamba na mfumo huo mpya.
Ameeleza kuwa mfumo huo wa Dijitali hauendeshwi na vifaa tu bali pia wafanya kazi waliopata mafunzo ya kutosha ndio watakaoweza kukabiliana na mfumo huo wa teknologia hivyo suala la kuwajengea uwezo wa mafunzo wafanyakazi ni la lazima.


















No comments:

Post a Comment