Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Deogratias Kessy wa banda la VETA Moshi, wakati akitembelea katika mabanda ya maonyesho ya maadhimisho ya Wiki ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, yaliyoanza leo, mkoani Tanga. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Kapteni Mstaafu, Chiku Galawa.
Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha VETA, Mkoa wa Tanga, baada ya kuwasili kwenye Viwanja vya Tangamano, kwa ajili ya kuzindua maadhimisho ya Wiki ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi leo mjini humo.
Makamu wa Rais, Dk. Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi na Mwasisi wa Chuo cha Gemmological and Jewelary Vocation cha Arusha, Peter Salla, kuhusu matumizi ya mawe ya madini, wakati akitembelea katika mabanda ya maonyesho alipozindua maadhimisho ya Wiki ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Kitaifa mkoani Tanga. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Kapteni Mstaafu, Chiku Galawa na wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa VETA, Mhandisi. Zebadiah Moshi.
Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akifunua mashine ya king’ora ili kuzindua rasmi maadhimisho ya Wiki ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, yaliyoanza leo Machi 19, Kitaifa mkoani Tanga.
No comments:
Post a Comment